WHO:Magonjwa yaliyoongoza kusababisha vifo barani Afrika 2017
Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) hivi karibuni imeeleza kuwa Virusi vya Ukimwi (VVU) na Malaria sio tena chanzo kikubwa cha vifo barani Afrika bali magonjwa yanayotokana na namna ya kuishi yaani ‘lifestyle’.
Magonjwa hayo ni kama kisukari, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, saratani na mengine ambayo hutokana na kula vyakula vyenye mafuta mengi, unywaji wa pombe uliopitiliza na uvutaji wa sigara uliopitiliza na mengineyo.
Imeelezwa pia kuwa magonjwa yanayotokana na maabukizi ya bakteria na virusi kwenye njia ya hewa kama na mapafu pia yameshika kasi katika kuongeza idadi ya vifo vinavyotokea barani na pia kuchangia asilimia 16 ya vifo vya watoto wa chini ya miaka 5 duniani kote.
Magonjwa mengine yaliyotajwa ni yale ya kuharisha ambayo huchangiwa kwa kasi sana na matumizi ya maji yasiyo safi na salama na uchafu wa mazingira.
Post a Comment