Lionel Messi kamvulia kofia Cristiano Ronaldo
Jina la staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika club ya Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo alirudi kwenye headlines baada ya kufanikiwa kufunga hat-trick yake ya nane ya UEFA Champions League na kuwa sawa na mpinzani wake wa siku zote Lionel Messi wa FC Barcelona.
Usiku huo Ronaldo alifanikiwa kufunga magoli matatu ya Juventus katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League dhidi ya Atletico Madrid katika ushindi wa 3-0, hivyo wakaingia robo fainali wakiwa nyumbani kwa ushindi wa jumla ya aggregate ya magoli 3-2, Lionel Messi ambaye nae ametinga robo fainali kwa kuitoa Lyon alizungumzia uwezo wa Ronaldo na kumsifia.
“Kitu Ronaldo alichofanya usiku wa jana ulikuwa ni surprise kubwa kwa sababu nilifikiri Atletico watafuzu na kuendelea hatua inayofuata lakini Juventus wamewashinda na Cristiano Ronaldo alikuwa na usiku wa maajabu na hat-trick”>>>Lionel Messi
Sasa inasubiriwa droo kuchezeshwa droo ya game za robo fainali na kuweza kufahamu Juventus atapangwa na timu gani na FC Barcelona atapangwa na timu gani, hadi sasa timu nane zilizofuzu UEFA Champions League kucheza hatua ya robo fainali ni FC Porto, Juventus, FC Barcelona, Ajax, Man United, Man City, Tottenham na Liverpool.
Umeona lakikini kaka Ile penalty haramu ya man united SASA anaenda Kufa Kwa Barcelona
ReplyDelete