MICHEZO Wachezaji wa Taifa Stars wanahitajika kambini March 17
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa sasa inatarajia kucheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi D wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2019 nchini Misri dhidi ya timu ya taifa ya Uganda The Cranes, mchezo wa mwisho wa Taifa utachezwa uwanja wa Taifa March 24.
Kocha mkuu wa kikosi hicho raia wa Nigeria Emmanuel Amunike ametangaza kikosi cha wachezaji 25 watakaoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo, wachezaji wote walioitwa na kocha Amunike sasa wataanza kuingia kambini March 17 2019.
Ratiba hiyo imetangazwa kwa kuzingatia wachezaji wa Simba pia wanaomalizia mchezo wao wa hatua ya Makundi wa michuano ya CAF Champions League, Taifa Stars inahitaji ushindi katika Kundi hilo ili iweze kufuzu kwa kuungana na Uganda ambao tayari wameshafuzu, kwani timu za Lesotho na Cape Verde nazo zina nafasi kama zitashinda game yao.
Post a Comment