Header Ads

MICHEZO PICHA: Aliyefunga goli la Tanzania kufuzu AFCON 1980 amekabidhiwa pesa



Wakati Rais Magufuli akiwapongeza na kuwazawadia viwanja wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa kusaidia timu hiyo kufuzu kucheza fainali za AFCON 2019kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39.

Rais Magufuli hakumsahau Peter Tino mchezaji ambaye aliifungia goli Taifa Stars na kufuzu kucheza fainali za AFCON 1980, kwa kumpa Tsh milioni 5 baada ya kumuita na kumuuliza anafanya shughuli gani kwa sasa na kusema kuwa hana kazi.



Baada ya kukabidhiwa pesa hizo Peter Tino akiambatana na meneja vifaa wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars John Mashaka na maafisa wa bank walimfungulia account kwa ajili ya kutunza pesa hizo.

No comments